| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Ukosefu wa hewa. Tazama Vidokezo.
|
Uingizaji hewa. Kinga ya kupumulia endapo ukolezi ni mkubwa.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu.
|
Ainisho ya EU Alama: F+ R: 12 S: (2-)-9-16-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G1F Msimbo wa NFPA : H 1; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Baridi. Uingizaji hewa kwenye sakafu na dari.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU AU ILIYOBANWA, ISO RANGI, ISO HARUFU. HATARI KWA MWILI: Gesi ni nyepesi kuliko hewa. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: Kinacho nyima pumzi sahili; (ACGIH 2000). MAK haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Isipodhibitiwa gesi hii huweza kusababisha kukosekana hewa kwa kupunguza kiasi cha oksijeni hewani katika maeneo funge. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -161°C Kiwango myeyuko: -183°C Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 3.3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.6 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 537°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5-15 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.09 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Uzito wa kioevu kwenye kiwango mchemko: 0.42 kg/l. Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Baada ya kutumia katika kulehemu, funga valvu; kagua neli, mara kwa mara n.k., na chunguza uvujaji kwa kutumia maji na sabuni. Hatua zilizotajwa katika sehemu ya KINGA zinahusu uzalishaji, ujazaji wa silinda, na uhifadhi wa gesi. Nambari za UN: 1972 Methane, refridgerated liquid (kioevu baridi mno) , Hazard class: 2.1.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||