MAGNESIUM (POWDER) ICSC: 0289
Aprili 2000

CAS # 7439-95-4 Mg
RTECS # OM2100000 Masi ya atomi: 24.30
UN # 1418
EC # 012-001-00-3 (pyrophoric)
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na unyevuunyevu, asidi, halojeni na dutu nyingine nyingi.
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine. USITUMIE maji.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa kichwa. Mazimbwezimbwe. Udhaifu. Homa au kuongezeka joto la mwili.


Ngozi


Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.

Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Kisichoingiza hewa.
Ainisho ya EU
Alama: F
R: 15-17
S: (2-)-7/8-43
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Jasara tanzu za UN: 4.2
Kikundi Ufungashaji cha UN: ll
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43GWS-II+III
Msimbo wa NFPA : H 0; F 1; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MAGNESIUM (POWDER) ICSC: 0289
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA KIJIVU

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa au unyevuunyevu kutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo mingi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na asidi na maji kutoa gesi yanayoweza kuwaka (hidrojeni tazama ICSC0001), kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kuvuta hewa yenye mafusho kunaweza kusababisha homa ya metali.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1100°C
Kiwango myeyuko: 651°C
Uzito wiani: 1.7 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Jotoridi la kujiwasha: 473°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: tazama Vidokezo
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Huwaka kwa mwale mkali sana. Ili kuzuia macho yasiumie usiangalie mwale wa magnesi bila kinga. Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji, dioksidi kaboni na poda. Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: (LEL) 0.03 kg/m³.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005