| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
Ona ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA.
|
EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 61-20/22-33-50/53-62 S: 53-45-60-61 Angalia: [A; E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-II
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEKUNDU HADI MANJANO HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana pamoja na poda ya alumini. Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama Pb 0.05 mg/m³; A3; (ACGIH 2002). MAK: kama Pb 0.1 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(8); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo mkuu wa neva, mfumo wa neva wa pembeni na mafigo, kusababisha anemia, adhari kwa ubongo (kama kifafa) (encephalopathy), ugonjwa wa neva wa pembeni, tumbo kuuma na kuharibika kwa figo. Husababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 1470°C Kiwango myeyuko: 888°C Uzito wiani: 9.5 g/cm³ Umumunyifu katika maji: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mimea na kwa mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Ona ICSC 0052 Lead.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||