HYDROGEN SELENIDE ICSC: 0284
Septemba 1993

Selenium hydride
(silinda)
CAS # 7783-07-5 H2Se
RTECS # MX1050000 Masi ya molekuli: 81.0
UN # 2202
EC # 034-002-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Udhaifu.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-33-50/53
S: (1/2-)-20/21-28-45-60-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2TF
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HYDROGEN SELENIDE ICSC: 0284
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 100°C huzalisha dutu yenye sumu na ziwakazo kama vile selenium (ICSC 0072) na hidrojeni (ICSC 0001). Dutu hii ni kitapasaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Inapogusana na hewa hutoa mafusho yenye sumu na babuzi (dioksidi seleniamu ICSC 0946).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: 0.015 ppm, 0.05 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi kunaweza kusababisha ugonjwa wa mapafu (pneumonitis). Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -41°C
Kiwango myeyuko: -66°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.1 (kama kioevu)
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 22.5°C: 270
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21°C: 878
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.8
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005