HYDROGEN FLUORIDE ICSC: 0283
Aprili 2000

Hydrofluoric acid, anhydrous
(silinda)
CAS # 7664-39-3 HF
RTECS # MW7875000 Masi ya molekuli: 20.0
UN # 1052
EC # 009-002-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kutapika. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozinzito. Malengelenge. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. Zirai.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+, C
R: 26/27/28-35
S: (1/2-)-7/9-26-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S1052 au 80GCT1-I
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HYDROGEN FLUORIDE ICSC: 0283
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI AU KIOEVU KISICHO RANGI, KIFUKACHO, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni asidi kali, humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo mingi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali, kioo, aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (as F) 0.5 ppm kama TWA, 2 ppm (kiwango cha juu); BEI imetolewa; (ACGIH 2005).
MAK: 2 ppm, 1.7 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; MAK: BAT 7 mg/g creatinine; (DFG 2005).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi au mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii yaweza kudukiza upungufu na kalsiamu ya damu (hypocalcemia). Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kusababisha mabadiliko kwa mifupa na meno kwa sababu ya florini (fluorosis).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 20°C
Kiwango myeyuko: -83°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.0 kioevu ifikapo 4°C
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 122
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.7
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Namba ya muungano wa mataifa (UN) kwa hidrojeni floraidi ya mmumunyo wa majimaji: 1790, ainisho ya hatari 8, jasara tanzu za UN 6.1, kikundi ufungashaji I (>60%).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005