| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na metali kama matokea ya kufanyiza hidrojeni.
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Ainisho ya EU Alama: C R: 35-37 S: (1/2-)-7/9-26-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1048 au 20G2TC Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0; |
Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA, YENYE HARUFU KALI. ISO RANGI HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo katika maji ni asidi kali humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na vitenzi vikaboni nyingi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC 0001). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 3 ppm; (kiwango cha juu kabisa) (ACGIH 2000). MAK: 2 ppm, 6.7 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -67°C Kiwango myeyuko: -87°C Uzito wiani (maji = 1): 1.8 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 193 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2445 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.8 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Nambari nyingine za UN: 1788 Asidi hidrobromiki (mmumunyo), ainisho ya hatari 8.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||