HYDRAZINE (anhidrasi) ICSC: 0281
Machi 1995

Diamide
Diamine
Nitrogen hydride
CAS # 302-01-2 N2H4 / H2N-NH2
RTECS # MU7175000 Masi ya molekuli: 32.1
UN # 2029
EC # 007-008-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 38°C. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na misombo mingi.
Mfumo funge wa zaidi ya 38°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Inababua. Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Degedege.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Inababua. YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
Macho Inababua. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Msokoto wa tumbo. Udhaifu. Kutapika. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Maunzi maalum. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-10-23/24/25-34-43-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 3 na 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S2029
Msimbo wa NFPA : H 3; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho (tazama Hatari za Kikemikali).
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HYDRAZINE (anhidrasi) ICSC: 0281
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI, KISICHO RANGI, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana huzalisha mafusho ya amonia, hidrojeni na oksidi za nitrojeni, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji. Dutu hii ni besi kali ya kati. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na metali nyingi, oksidi ya metali na vitu vinavyoruhusu vimiminika kupita kwa urahisi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Kumenyuka hakuhitaji kuwepo kwa hewa au oksijeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.01 ppm kama TWA; (ngozi); A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); kuhisisha ngozi (Sh); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho na ngozi. Mvuke huu ya dutu hii husababisha ulikaji kwa njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo na mfumo mkuu wa neva. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo na mfumo mkuu wa neva. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 114°C
Kiwango myeyuko: 2°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.01
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 38°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: tazama Vidokezo
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-100
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -3.1
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Jotoridi la kuwaka yenyewe linabadilika kuanzia 24°C kwa nyuso za vyuma zenye kutu hadi 270°C kwa nyuso za kioo. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Nambari nyingine za UN: UN 2030 Hidrati hidrazini au Hidrazini, mmumunyo kwa hidrazini 37-64% na maji; UN 3293 Hidrazini, mmumunyo na maji usiozidi hidrazini 37%.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005