ETHYL ACRYLATE ICSC: 0267
Novemba 2003

2-Propenoic acid, ethyl ester
Acrylic acid ethyl ester
Ethyl propenoate
Akrilati ethili
CAS # 140-88-5 CH2CHCOOC2H5 / C5H8O2
RTECS # AT0700000 Masi ya molekuli: 100.1
UN # 1917
EC # 607-032-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Mavazi ya kinga. Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn
R: 11-20/21/22-36/37/38-43
S: (2-)-9-16-33-36/37
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1917
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Baridi. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYL ACRYLATE ICSC: 0267
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. Mvuke haina kuzuisi na yaweza kuwa polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi na kufunga tundu.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha mara moja yenyewe kutokana na kupata joto kwa kuathiriwa na mwanga na inapogusana na peroksaidi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA, 15 ppm kama STEL; A4; (ACGIH 2003).
MAK: 5 ppm 21 mg/m³; Sh; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Tezi zimeonekana katika majaribio ya wanyama lakini huweza isiwe hivyo kwa binadamu (tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 99°C
Kiwango myeyuko: -71°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.92
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.5
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 3.9
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.45
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.09
Kiwango cha kumweka: 9°C (c.c.)
Jotoridi la kujiwasha: 345°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-14
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.32
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005