DODECANOYL PEROXIDE ICSC: 0264
Machi 1999

Lauroyl peroxide
Peroxide, didodecanoyl
bis(1-Oxododecyl) peroxide
CAS # 105-74-8 (C11H23CO)2O2
RTECS # OF2625000 Masi ya molekuli: 398.7
UN # 3106
EC # 617-003-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Maji mengi, mnyunyizo wa maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka, vinakisishaji na inapopata joto.
Zuia ukanzaji zaidi ya 25° C.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari endapo mwagigo ni mwingi. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: O
R: 7
S: (2-)-3/7-14-36-37/39
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 52GP1-S
Msimbo wa NFPA : H 0; F 2; R 3; OX
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DODECANOYL PEROXIDE ICSC: 0264
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE AU MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Erosoli hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 49-57°C
Uzito wiani: 0.9 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Jotoridi la kujiwasha: 112°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Laurox W 40, Alperox, LYP97 ni majina ya kibiashara. Nambari nyingine za UN, mmumunyo wa maji (<42%): 3109.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005