1,2-DIPHENYLHYDRAZINE ICSC: 0263
Aprili 2005

Hydrazobenzene
Diphenylhydrazine
N,N'-Bianiline
CAS # 122-66-7 C12H12N2 / C6H5NHNHC6H5
RTECS # MW2625000 Masi ya molekuli: 184.3
UN #
EC # 007-021-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO Tazama ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA.
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-22-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,2-DIPHENYLHYDRAZINE ICSC: 0263
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE HADI MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na asidi minerali kusababisha benzidini (tazama ICSC0224).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembeya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Yaweza kusababisha muwasho wa mekaniko.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 125-131°C
Uzito wiani: 1.16 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: <0.1 mbaya
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.94
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005