DIMETHYLAMINE ICSC: 0260
Mei 2003

Methanamine, N-methyl
DMA
(silinda)
CAS # 124-40-3 (CH3)2NH / C2H7N
RTECS # IP8750000 Masi ya molekuli: 45.1
UN # 1032
EC # 612-001-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Alama: F+, Xn
R: 12-20-37/38-41
S: (2-)-16-26-39
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1032
Msimbo wa NFPA: H 3; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIMETHYLAMINE ICSC: 0260
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI YENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na zebaki kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia shaba, aloi za zinki, alumini, uso ulipakwa madini, na plastiki. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji, ona ICSC 1485 Dimethylamine, mmumunyo wa maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA; 15 ppm kama STEL; A4; (ACGIH 2003).
EU OEL: 2 ppm, 3.8 mg/m³ kama TWA; 5 ppm, 9.4 mg/m³ kama STEL; (EU 1998).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi wa viwango vya juu ya dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 7.0°C
Kiwango myeyuko: -92.2°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.7
Umumunyifu katika maji: 354 g/100ml
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 203
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.6
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 400°C°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.8-14.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.2
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Ona ICSC 1485 Dimethylamine, mmumunyo wa maji.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005