N,N-DIMETHYLACETAMIDE ICSC: 0259
Septemba 1993

Acetic acid dimethylamide
Dimethylacetamide
CAS # 127-19-5 CH3CON(CH3)2
RTECS # AB7700000 Masi ya molekuli: 87.1
UN #
EC # 616-011-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 70°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 70°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.

MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho MWUKE UTAFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuhara. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 61-20/21
S: 53-45
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 0;
Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
N,N-DIMETHYLACETAMIDE ICSC: 0259
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KAMA MAFUTA, KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Hushambulia plastiki nyingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm kama TWA; (ngozi); A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2004).
MAK: 10 ppm, 36 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 165°C
Kiwango myeyuko: -20°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.94
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.33
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.01
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 70°C (o.c.)
Jotoridi la kujiwasha: 490°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8 (ifikapo 100°C) - 11.5 (ifikapo 160°C)
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.77
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa udongo.
VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Ufonzaji kupitia kwenye ngozi huendelea haraka sana. Aina nyingi za glavu za kinga hazizuii kikamilifu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005