| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kuzinzia. Mazimbwezimbwe Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Ukwaru.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. (Zaidi tazama Uvutaji pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: F, Xn R: 11-22-36/37-52/53 S: (2-)-16-23-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-I+II Msimbo wa NFPA : H 2; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na: tazama Hatari za Kikemikali. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (ikiwa ni) pamoja na fosjini (tazama ICSC 0007) na kloridi hidrojeni (ICSC 0163). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, metali alkali na alkaliardhi, metali unga, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia alumini, feri na polyethilini. Mgusano na kibabuzi kikali waweza kusababisha uundaji wa gesi iwakayo na yenye sumu ya asetalidehide. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 100 ppm kama TWA; A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2004). MAK: 100 ppm, 410 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa kiwango cha juu huweza kusababisha kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 57°C Kiwango myeyuko: -98°C Uzito wiani (maji = 1): 1.2 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.6 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 24 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4 |
Kiwango cha kumweka: -6°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 458°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.6-11.4 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.8 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||