| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji na maunzi yasiokubaliana (ona Hatari za Kikemikali).
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mchomo. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Inababua. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: F, T+, N R: 11-24/25-26-37/38-41-48/22-50-68 S: (1/2-)-26-28-36/37/39-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF1-I Msimbo wa NFPA: H 4; F 3; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI. HUGEUKA NJANO ISIYOKOZA INAPOFIDULIWA NA MWANGA NA HEWA. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kwa athari ya moto au mlipuko. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji na dutu nyingine nyingi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki na dutu nyingine nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.3 ppm; (Kiwango cha juu); (ngozi); A3; (ACGIH 2003). MAK: H; Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Inayotoza machozi. Mvuke huu inakera kwa ukali ngozi, njia ya upumuaji, husababisha ulikaji kwa macho. Kuvuta pumzi wa viwango vya juu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi wa viwango vya juu kunaweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 104°C Kiwango myeyuko: (trans) -76.5; (cis) -69°C Uzito wiani (maji = 1): 0.85 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 15-18 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 4.0 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.41 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.06 Kiwango cha kumweka: 13°C o.c. Jotoridi la kujiwasha: 232.2°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.1-15.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.63 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama. Crotonaldehyde iliyomarishwa kwa maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||