2-CHLOROETHANOL ICSC: 0236
Mei 2003

2-Chloroethyl alcohol
Ethylene chlorohydrin
Glycol chlorohydrin
CAS # 107-07-3 C2H5ClO / ClCH2CH2OH
RTECS # KK0875000 Masi ya molekuli: 80.5
UN # 1135
EC # 603-028-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 60°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 60°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 26/27/28
S: (1/2-)-7/9-28-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1135
Msimbo wa NFPA: H 4; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na besi kali, vioksidishaji, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-CHLOROETHANOL ICSC: 0236
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi (kloridi hidrojeni, fosjini). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na maji au mvuke kuzalisha mafusho yenye babuzi na sumu. Humenyuka pamoja na besi kali kusababisha oksidi ethilini, kusababisha athari yenye sumu na ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm (Kiwango cha juu), (ngozi); A4; (ACGIH 2003).
MAK: 1 ppm, 3.3 mg/m³; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: II(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mfumo wa moyo na mishipa, mafigo na ini kusababisha ugonjwa wa moyo, kuanguka kwa shinikizo ya damu, kuharibika kwa figo, kuharibika kwa ini na kutoweza kupumua. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 128-130°C
Kiwango myeyuko: -67°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.65
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.78
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 60°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 425°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4.9-15.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.06
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005