CHLOROACETIC ACID ICSC: 0235
Mei 2003

Chloroethanoic acid
Monochloroacetic acid
MCA
CAS # 79-11-8 C2H3ClO2 / ClCH2COOH
RTECS # AF8575000 Masi ya molekuli: 94.5
UN # 1751
EC # 607-003-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kutapika. Degedege. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia. Degedege. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 25-34-50
S: (1/2-)-23-37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1751
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na besi kali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CHLOROACETIC ACID ICSC: 0235
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI, RISHAI, YENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na kloridi hidrojeni, fosjini. Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati. Hushambulia metali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo) (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya erosoli kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo mkuu wa neva kusababisha ugonjwa wa moyo, degedege na kuharibika kwa figo. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 189°C
Kiwango myeyuko: ona Vidokezo
Uzito wiani: 1.58
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 8.68
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.26
Kiwango cha kumweka: 126°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 470°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 8 -?
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.34
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kiwangp myeyuko: ikiwa isoma alpha = 63°C, beta = 56.2°C, au gamma = 52.5°C. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Namba nyingine za UN: 1750 Asidi kloroasetiki, mmumunyo; 3250 Asidi kloroasetiki, katika hali ya myeyuko.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005