| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kusinzia. Kupoteza fahamu.
|
Mfumo funge na uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
|
Ainisho ya EU Alama: F+ R: 12 S: (2-)-9-16-33 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1011 Msimbo wa NFPA: H 1; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO HARUFU, ISO RANGI HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 800 ppm kama TWA; (ACGIH 2003). MAK: 1000 ppm, 2400 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(4); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2003). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -0.5°C Kiwango myeyuko: -138°C Uzito wiani (maji = 1): 0.6 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.0061 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21.1°C: 213.7 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.1 |
Kiwango cha kumweka: -60°C Jotoridi la kujiwasha: 365°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-8.4 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.89 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Maelezo isipokuwa muundo pia yanahusu Isobutane (CAS 75-28-5). Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||