| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Inababua. Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mchomo. Maumivu. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kinga. Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa mafusho kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: T+, C R: 14-26-35 S: (1/2-)-9-26-28-36/37/39-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G1TC
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na metali alkali, metaliardhi ya alkali, alkili nitrati na chokaa. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI ISO RANGI, ILIYOBANWA YENYE HARUFU KALI. INATOA MAFUSHO MEUPE KATIKA HEWA. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hupolimisha misombo isokefu. Dutu hii hutengana inapogusana na maji na unyevu, huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile floridi hidrojeni (tazama ICSC 0283), asidi floroboroni asidi boroni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na metali kama vile sodiamu, potasiamu na kalsium, na pamoja na alkili nitrati. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm (kiwango cha juu); (ACGIH 2004). MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Hubabua. Inayotoza machozi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mafigo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -100°C Kiwango myeyuko: -127°C Umumunyifu katika maji: mmenyuko (tazama vidokezo) Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.4 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Trifloridi boroni inayeyuka kwenye maji baridi, gramu 332/mililita 100 kwenye joto digrii 0°C. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya saa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||