| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Udhaifu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Mtambo wa kutolea nje. Kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kwa uangalifu zolea mwagigo kwenye kiwekeo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T+ R: 49-25-26-36/37/38-43-48/23 S: 53-45 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 4.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF3-II Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na asidi kali, besi, vimumunyishaji vyenye klorini, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA KIJIVU HADI NYEUPE HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka pamoja na asidi kali na besi kali kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001). Ikiwa vimumunyisho vyenye klorini, kama vile tetrakloridi kaboni na trikloroethilini hutoa michanganyiko isiyohimili mshtuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.002 mg/m³ kama TWA; 0.01 mg/m³ as STEL; A1 (imethibitishwa kuwa kasijeni kwa binadamu); (ACGIH 2004). MAK: uhisishaji wa koromeo la hewa na ngozi (Sah); Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Erosoli hii inakera njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye vumbi au mafusho kunaweza kusababisha kuvimba wa mapafu kunakutokana na kemikali. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa chembe za vumbi, kusababisha ugonjwa sugu wa berili (kikohozi, kupungua uzito, udhaifu). Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: zaidi ya 2500°C Kiwango myeyuko: 1287°C Uzito wiani: 1.9 g/cm³ Umumunyifu katika maji: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||