ARSENIC TRICHLORIDE ICSC: 0221
Aprili 2000

Arsenic III chloride
Arsenous chloride
CAS # 7784-34-1 AsCl3
RTECS # CG1750000 Masi ya molekuli: 181.2
UN # 1560
EC # 033-002-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na maji na metali.
Moto unapotokea katika eneo: USITUMIE maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipukomaji na metali.


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo plastiki vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-50/53
S: (1/2-)-20/21-28-45-60-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-61GT4-I
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Baridi. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ARSENIC TRICHLORIDE ICSC: 0221
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KAMA MAFUTA, KIFUKACHO, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163) na oksidi za arseniki. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na unyevuunyevu au maji kutoa kloridi hidrojeni. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC#0001).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.01 mg/m³ kama TWA; A1 (imethibitishwa kuwa kasijeni kwa binadamu); BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera sana macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa moyo na mishipa, mfumo mkuu wa neva, kusababisha uvimbe wa tumbo na chango, upungufu wa maji na eletroliti mwilini, ugonjwa wa moyo, mshtuko, degedege. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri kiwamboute, ngozi, mfumo wa neva wa pembeni, ini na uboho, kusababisha kugeuka kwa rangi ya asili, ugumu wa ngozi, vitobo vya tenganisho la pua, uvimbe wa neva, kuharibika kwa ini na anemia. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii inaweza kusababisha ulemavu kwa watoto wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 130.2°C
Kiwango myeyuko: -16°C
Uzito wiani: 2.1 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.17
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.06
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa udongo, viumbe hai vya majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kiwango myeyuko dhahiri kinachosababishwa na upoteaji wa maji fuwele kimeelezwa. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005