ANTIMONY PENTAFLUORIDE ICSC: 0220
Machi 1995

Antimony(V) fluoride
CAS # 7783-70-2 SbF5
RTECS # CC5800000 Masi ya molekuli: 216.8
UN # 1732
EC # 051-003-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Poda, dioksidi kaboni, USITUMIE vitenzi vya majimaji. USITUMIE maji.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Inabaua. Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mibabuko ya ngozi nzito. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu. Paka glukunati kalsiamu sehemu zilizoungua.
Macho Inababua. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 20/22
S: (2-)
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GCT1-II+III
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 1;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANTIMONY PENTAFLUORIDE ICSC: 0220
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI, KISICHO RANGI, KAMA MAFUTA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi, na hata stibi na florini. Humenyuka vikali ikiwa na maji kufanyiza mafusho yenye sumu na babuzi floridi hidrojeni (tazama ICSC 0283). Hushambulia kioo, shaba na risasi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama Sb) 0.5 mg/m³ kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: (kama Sb) Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2005).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri damu, msuli ya moyo, mafigo na ini, kusababisha ugonjwa wa moyo na kuharibika kwa utendaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 141°C
Kiwango myeyuko: 8.3°C
Uzito wiani (maji = 1): 3.00
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 1.33
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji au vitenzi vya majimaji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Pia shauriana na ICSC #0283 (Floridi hidrojeni).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005