sec-AMYL ACETATE ICSC: 0219
Aprili 2000

2-Pentyl acetate
Acetic acid, 2-pentyl ester
1-Methylbutyl acetate
CAS # 626-38-0 C7H14O2 / CH3COOCH(CH3)C3H7
RTECS # AJ2100000 Masi ya molekuli: 130.2
UN # 1104
EC # 607-130-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 32°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 32°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
R: 10-66
S: (2-)-23-25
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: 30S1104 au 30GF1-III
Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
sec-AMYL ACETATE ICSC: 0219
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki nyingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA; 100 ppm kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: 50 ppm, 270 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kupungua kwa fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 121°C
Kiwango myeyuko: -148°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.86
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.93
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 32°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 380°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.0-7.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.26
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005