| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Kilipukaji. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na vitenzi vinavyoweza kuwaka na vinakisishaji.
|
Maji mengi. HAKUNA vitenzi zimishi vingine. Moto unapotokea katika eneo: tumia kiazi kikubwa cha maji kwenye hatua za mwanzo.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapokuwa imefungwa na iwapo na halijoto kubwa.
|
|
Ondoka katika eneo la hatari. Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Degedege. Kuhara. Kizunguzungu. Kutapika. Udhaifu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo visivyowaka. Osha salio kwa maji mengi.
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-51S1942 au 51GO2-I+II+III Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 3; ox |
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, ISO RANGI, A RISHAI HADI NYEUPE. HATARI ZA KIKEMIKALI: Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Dutu hii hutengana inapokanzwa au huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo takribani 210°C Kiwango myeyuko: 170°C Uzito wiani: 1.7 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 190 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Huwa nyepesi kushtuka ikichanganyika na maunzi kikaboni. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||