AMMONIUM HYDROXIDE (10%-35% solution) ICSC: 0215
Machi 1995

Aqua ammonia
Ammonium hydrate
CAS # 1336-21-6 NH4OH
RTECS # BQ9625000 Masi ya molekuli: 35.1
UN # 2672
EC # 007-001-01-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Tazama Vidokezo.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia. Kilichofungwa viwekeo vizuri.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Inababua. Wekundu. Mibabuko ya ngozi nzito. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inababua. Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Kuumwa koo. Kutapika. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam endapo kiasi kikubwa kimemwagika. Uingizaji hewa. Katisha kioevu kilichomwagika kwa uangalifu kwa asidi iliyozimuliwa, kama vile asidi sulfuriki iliyozimuliwa. Osha salio kwa maji mengi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: C, N
R: 34-50
S: (1/2-)-26-36/37/39-45-61
Angalia: [B]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S2672
Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
AMMONIUM HYDROXIDE (10%-35% solution) ICSC: 0215
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MMUMUNYO UVUKAO SANA WA AMMONIA WA MAJI, USIO RANGI, WENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na metali nzito nyingi na chumvi zake kufanyiza misombo lipukaji. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC 0001). Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, inamenyuka kwa ukali sana na asidi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (gesi NH_3) 25 ppm kama TWA; 40 ppm kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: 20 ppm, 14 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake au aerosol na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi yenye kiwango kikubwa cha mvuke kunaweza kusababisha kuvimba wa koo na mibabuko katika njia ya kupumulia, na kichomi. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa mvuke au erosoli.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: (25%) 38°C
Kiwango myeyuko: (25%) -58°C
Uzito wiani (maji = 1): (25%) 0.9
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: (25%) 48
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.6-1.2
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Katika hali fulani mvuke wa amonia unaweza kuwaka na kulipuka. Ufahamu kuwa gesi ya amonia yaweza kufuka kutoka kwenye mmumunyo wa amonia. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usijaze chupa na dutu hii hadi juu, mimumunyo mikali yaweza kusababisha msukumo. Fungua kwa uangalifu. Nambari nyingine za UN ni UN 1005 Amonia, anhidrasi kimiminika au mmumunyo wa amonia, uzito wiani wa pungufu ya 0.880 katika 15°C kwenye maji, ikiwa na amonia zaidi ya 50%; UN 2073 Amonia, 35-50%. Pia shauriana na ICSC #0414 Amonia.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005