| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Udhaifu.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT2-II
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vioksidishaji vikali, asidi kali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA AU FUWELE ZISIO NA RANGI AU NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha oksidi za nitrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.5 ppm kama TWA; (ACGIH 2004). MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege, matatizo ya kupumua. Dutu hii huweza kusababisha ongezeko la msukumo wa damu. Mfiduo juu ya OEL huweza kusababisha kifo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 211°C Kiwango myeyuko: 58°C Umumunyifu katika maji: vizuri sana Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0.8 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.2 |
Kiwango cha kumweka: 68°C c.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.49 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Uhusiano baina ya harufu na kikomo cha mfiduo wa kazi hauwezi kuonyeshwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||