| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kutapika. Tazama Vidokezo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2205 au 61GT1-III Msimbo wa NFPA : H 4; F 2; R 1; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI AU HARUFU, KAMA MAFUTA, HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu sana (sianidi hidrojeni ICSC 0492). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 ppm kama TWA; (ngozi); (ACGIH 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Mfiduo huweza kusababisha degedege. Mfiduo huweza kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri damu na adrenali, kusababisha anemia na vidonda vya tishu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 295°C Kiwango myeyuko: 1°C Uzito wiani (maji = 1): 0.97 Umumunyifu katika maji: wastani Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Kiwango cha kumweka: 159°C c.c. (tazama Vidokezo) Jotoridi la kujiwasha: 550°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.7-4.9 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.32 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Huduma ya kwanza maalum na matibabu ni muhimu endapo umedhuriwa na sumu ya adiponitrile. Mshauri daktari. Kiwango cha kumweka cha adiponitrile, gredi ya kiteknikali ni 93°C (o.c.). Usichukue nguo za kazi nyumbani. Pia shauriana na ICSC #0492.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||