ACETIC ANHYDRIDE ICSC: 0209
Septemba 1993

Acetic acid, anhydride
Acetic oxide
Ethanoic anhydride
Acetyl oxide
CAS # 108-24-7 C4H6O3 / (CH3CO)2O
RTECS # AK1925000 Masi ya molekuli: 102.1
UN # 1715
EC # 607-008-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni. (Tazama Vidokezo).
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 49°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 49°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Inababua. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Inababua. Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inababua. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Maumivu ya tumbo. Kuumwa koo. Kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 10-20/22-34
S: (1/2-)-26-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S1715 au 80GCF1-II
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 1; W
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACETIC ANHYDRIDE ICSC: 0209
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, NYEPESI KUMIMINIKA CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha gesi na mafusho yenye sumu kama vile asidi asetiki. Humenyuka vikali ikiwa na maji yanayochemka, mvuke, vioksidishaji vikali, alkoholi, amini, besi kali na dutu nyingine nyingi. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. Hiki ni kioevu babuzi kikali, hasa kwenye maji au unyevyunyevu (zaidi tazama Vidokezo).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA (ACGIH 2004).
MAK: 5 ppm, 21 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Hubabua. Inayotoza machozi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 139°C
Kiwango myeyuko: -73°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.08
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 49°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 316°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.7-10.3
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Inapochanganywa na maji hutoa asidi asetiki. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya saa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Mioto mikubwa lazima izimwe kwa kiasi kikubwa cha maji yanayotokea mbali.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005