ZINC OXIDE ICSC: 0208
Aprili 2004

Zinc white
Zinc monoxide
C.I. Pigment White 4
CAS # 1314-13-2 ZnO
RTECS # ZH4810000 Masi ya molekuli: 81.4
UN #
EC # 030-013-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Homa au muinuko wa hali ya joto. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. Baridi kali. Maumivu wa misuli. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Alama: N
R: 50/53
S: 60-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI


IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ZINC OXIDE ICSC: 0208
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na pamoja na poda za alumini na magnesiamu, na unapokanzwa pamoja na mpira wenye klorini kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (sehemu pumuzi) 2 mg/m³ kama TWA; (ACGIH 2004).
TLV: (sehemu pumuzi) 10 mg/m³ kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: (kama vumbi) (sehemu pumuzi), 1 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka; hasa iwapo katika hali ya vumbi (zinc oxide fume particles).

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kuvuta hewa yenye mafusho kunaweza kusababisha homa ya metali. Dutu hii inakera kama vumbi njia ya upumuaji. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 1975°C
Uzito wiani: 5.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za homa ya metali hazijitokezi mpaka baada ya saa kadhaa kupita.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005