| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F+, Xn R: 12-20-37/38-41 S: (2-)-16-26-39 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1083 Msimbo wa NFPA: H 3; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji, ethilini oksidi. Hushambulia metali kama vile shaba, zinki, alumini, bati, na aloi zake. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 ppm (kama TWA); 15 ppm (kama STEL); (ACGIH 2002). MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Kuvuta pumzi yenye dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 3°C Kiwango myeyuko: -117°C Uzito wiani (maji = 1): 0.6 (kioevu) Umumunyifu katika maji: vizuri sana Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 187 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 190°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.0-11.6 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.2 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo (MAK IIb).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||