PROPYLENE OXIDE ICSC: 0192
Machi 1995

1,2-Epoxypropane
Methyloxirane
Methyl ethylene oxide
Propene oxide
CAS # 75-56-9 CH3CHCH2O / C3H6O
RTECS # TZ2975000 Masi ya molekuli: 58.1
UN # 1280
EC # 603-055-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: F+, T
R: 45-46-12-20/21/22-36/37/38
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1280 au 30GF1-I-II
Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na asidi, besi, vioksidishaji. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PROPYLENE OXIDE ICSC: 0192
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI VUKIVU SANA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha kwa ukali kwa kuathiriwa na besi, asidi na kloridi ya metali kwa athari ya moto au mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na klorini, amonia, vioksidishaji vikali, asidi kusababisha athariya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA; A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); SEN; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 34°C
Kiwango myeyuko: -104°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 40.5
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 59
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.0
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.6
Kiwango cha kumweka: -37°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 449°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-38.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.03
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005