| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka katika hali mahususi. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko ikiwa michanganyiko vyenye vimumunyisho huweza kuwaka/kulipuka.
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Msongo/mfinyo (wa jicho). Kiwaa.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Degedege. Kuhara. Udhaifu. Kutetemeka misuli. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 25-50/53 S: (1/2-)-37-45-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT7-III
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile methili isosianeti, oksidi za nitrojeni. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.5 mg/m3 (ACGIH 1993) TLV: 0.5 mg/m³ kamaTWA; A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: (sehemu ndogo ya kuvutwa mapafuni) 2 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(8); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, ini, mafigo, kusababisha kutoweza kupumua, degedege na vidonda vya tishu. Kizuio cha kolinesterasi. Mfiduo huweza kusababisha kifo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: 91°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: (mbaya) 0.2 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.001 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.52 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mamalia, ndege, viumbe hai vya majini, viumbe viishivyo ardhini na nyuki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Baygon, Blattanex, Bolfo, Invisi-Gard, Isocarb, o-IMPC, Propyon, Rhoden, Sendran, Suncide, Tendex, Tugon Fliegenkugel, Unden, Undene ni majina ya kibiashara. Usitapishe iwapo zao limezimuliwa na vimumunyishaji vya kikaboni.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||