2-NITROPROPANE ICSC: 0187
Machi 1995

Isonitropropane
Dimethylnitromethane
sec-Nitropropane
CAS # 79-46-9 C3H7NO2 / CH3CHNO2CH3
RTECS # TZ5250000 Masi ya molekuli: 89.1
UN # 2608
EC # 609-002-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni,
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 24°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 24°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari endapo mwagiko ni mwingi. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-10-20/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-30GF1-III
Msimbo wa NFPA : H 2; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na besi kali, asidi kali, amini.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-NITROPROPANE ICSC: 0187
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KAMA MAFUTA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha oksidi za nitrojeni. Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa asidi, amini, besi iso-kikaboni na oksidi za metali nzito. Humenyuka pamoja na mkaa kusababisha athari ya moto. Yaweza kumenyuliwa na mkaa ulioamilishwa uliyoko katika chujio za kinga ya kupumulia.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm kama TWA; A3; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu yenye dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kuharibika kwa ini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini na mfumo wa neva, kusababisha kichefuchefu, kutapika, kuhara, kupungua hamu ya kula (anorexia) na kuumwa kichwa kikali. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 120°C
Kiwango myeyuko: -93°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.99
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 25°C: 1.7
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.7
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.04
Kiwango cha kumweka: 24°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 428°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.6-11
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.93
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. NiPar S-20 na NiPar S-30 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005