NITROGLYCERIN ICSC: 0186
Machi 1995

Glyceryl trinitrate
Glycerol trinitrate
1,2,3-Propanetriol trinitrate
Blasting oil
CAS # 55-63-0 C3H5N3O9 / C3H5(NO3)3
RTECS # QX2100000 Masi ya molekuli: 227.1
UN # 0143 (imezuiwa)
EC # 603-034-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Kilipukaji. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Msokoto wa tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya mwasho. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: E, T+, N
R: 3-26/27/28-33-51/53
S: (1/2-)-33-35-36/37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 1.1D
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 10G1.1
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 4;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITROGLYCERIN ICSC: 0186
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI TO MANJANO, KINATACHO AU FUWELE MANJANO ISIYOKOZA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu yanayoyumuisha oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na ozoni kusababisha athariya mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm; 0.46 mg/m³ TWA (ngozi) (ACGIH 1994-1995).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na damu, kusababisha kupungua msukumo wa damu na kufa kwa mzunguko na, kwa viwango vikubwa, kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Mfiduo unaorudiwa huishia kuleta usugu. Kuondoka kidogo kwenye mfiduo kwaweza kuishia kwenye kifo cha ghafia.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: kulipuka
Kiwango myeyuko: 13°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.6
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.03
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.8
Jotoridi la kujiwasha: 270°C
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Mwako katika nafasi funge huenda ukageuka kuwa mpasuko. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Nambari nyingine za UN: UN 0144: nitrogliserini, mmumunyo wa alkoholi na nitrogliserini zaidi ya 1% lakini siyo zaidi ya 10%; UN ainisho ya hatari 1.1D. UN 1204: mmumunyo wa alkoholi na nitrogliserini isiyozidi 1%; UN ainisho ya hatari 3, daraja fungasho II. UN 3064: mmumunyo wa alkoholi na nitrogliserini zaidi ya 1% lakini siyo zaidi ya 5%, UN ainisho ya hatari 3, daraja fungasho II.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005