SODIUM NITRATE ICSC: 0185
Oktoba 2001

Chile saltpeter
CAS # 7631-99-4 NaNO3
RTECS # WC5600000 Masi ya molekuli: 85
UN # 1498
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka na vinakisishaji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vinakisishaji.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Degedege. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kuchanganyikiwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vya plastiki au kioo. Osha salio kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51S1498
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM NITRATE ICSC: 0185
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha oksidi za nitrojeni na oksijeni, ambayo huongeza athari ya moto. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini ikimezwa. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 380°C
Kiwango myeyuko: 308°C
Uzito wiani: 2.3 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 92.1
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005