| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji vikali. Usigusishe na nyuso za moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji na oksidi za metali.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kichefuchefu. Kutapika. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Degedege. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 na 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTFC-I Msimbo wa NFPA: H 4; F 3; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, oksidi za metali, vitu vinavyoruhusu hewa, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika gesi ajizi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KIRISHAI, KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kulipuka wakati wa kukanza au inapogusana na oksidi za metali. Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa na maunzi yanayoruhusu hewa kama vile udongo, asbestosi, mkao au nguo. Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi pamoja na oksidi za nitrojeni. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto. Dutu hii ni besi kali ya kati na humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.01 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2004). MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); kuingia kupitia kwa ngozi (H); kuhisisha ngozi (Sh); (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, ini na damu kusababisha kuharibika kwa ini na kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ini na damu kusababisha kuharibika kwa ini na kufanyika kwa methemoglobini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 87.5°C Kiwango myeyuko: -52.4°C Uzito wiani (maji = 1): 0.87 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 4.8 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.6 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03 Kiwango cha kumweka: -8.3°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 196°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.5-97 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.05 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||