METHYLAMINE ICSC: 0178
Oktoba 2002

Methanamine
Aminomethane
Monomethylamine
(silinda)
CAS # 74-89-5 CH5N / CH3NH2
RTECS # PF6300000 Masi ya molekuli: 31.1
UN # 1061 (anhidrasi)
EC # 612-001-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Tazama Vidokezo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: F+, Xn
R: 12-20-37/38-41
S: (2-)-16-26-39
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1061
Msimbo wa NFPA: H 3; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYLAMINE ICSC: 0178
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. Hushambulia plastiki, mpira na mipako. Hushambulia shaba, zinki na aloi zake, alumini na uso ulipakwa madini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama TWA) 5 ppm; (kama STEL) 15 ppm; (ACGIH 2002).
MAK: 10 ppm, 13 mg/m³; (DFG 2002).
Ainisho ya MAK: Aina ya kiwango cha juu: I (1) viwango vya juu kabisa; Aina ya mimba: IIc; (2002)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya dutu hii wa viwango vya juu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -6°C
Kiwango myeyuko: -93°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.7 (kioevu)
Umumunyifu katika maji: katika 25°C vizuri sana
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 304
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.07
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 430°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4.9-20.7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.71
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005