MANEB ICSC: 0173
Novemba 2003

Manganese, ethylenebis(dithiocarbamato)
((1,2-Ethanediylbis(carbamodithioato))(2-))manganese
Manganese ethylene-1,2-dithiocarbamate
CAS # 12427-38-2 C4H6N2S4.Mn
RTECS # OP0700000 Masi ya molekuli: 265.3
UN # 2210
EC # 006-077-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na maji.
Dioksidi kaboni, poda kavu. USITUMIE vitenzi vya majimaji. USITUMIE maji.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 37-43
S: (2-)-8-24/25-46
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2
Jasara tanzu za UN: 4.3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 42S2210
Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MANEB ICSC: 0173
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU FUWELE MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapogusana na asidi na unyevu huzalisha gesi yanayoweza kuwaka na yenye sumu pamoja na sulfidi hidrojeni na disulfidi kaboni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: Sh; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na mfumo mkuu wa neva kusababisha kuharibika kwa figo na matatizo kwenye mishipa ya fahamu (manganism).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo 192-204°C
Uzito wiani: 1.92 g/cm³
Umumunyifu katika maji: ni dhaifu
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Namba za UN 2968: ainisho ya hatari 4.3; daraja fungasho III; Maneb iliyoimarishwa ili isijikanze yenyewe. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Chloroble M, Dithane M 22, Kypman 80, Manebgan, Manesan, Manzate, Polyram M, Rhodianebe, Sopranebe na Trimangol ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005