| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko ikiwa michanganyiko vyenye vimumunyisho huweza kuwaka/kulipuka.
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. Msokoto wa tumbo. Kutapika. Kuhara. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn R: 22 S: (2-)-24 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 9 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU MANJANO HADI KAHAWIA ILIYOKOZA (KUTEGEMEANA NA UBORA), CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za fosforasi na oksidi za sulfuri. Humenyuka vikali ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia feri na baadhi ya metali nyingine, baadhi ya plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 10 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1994) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, kusababisha degedege, kutoweza kupumua. Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 0.093kPa: 156-157°C Kiwango myeyuko: 3°C Uzito wiani (maji = 1): 1.2 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 30°C: 0.0053 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 11.4 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.89 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa nyuki. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za sumu kali hazijitokezi mpaka kabla ya dakika 30 au saa 1-2. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Carbofos, Celthion, Cythion, Emmatos, Fosfothion, Fyfanon, Karbofos, Kypfos, Malamar, Malatol, Malatox, Sadophos, Sumitox, Zithiol ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||