ISOPROPYL GLYCIDYL ETHER ICSC: 0171
Novemba 1998

1,2-Epoxy-3-isopropoxypropane
IGE
(Isopropoxymethyl)oxirane
CAS # 4016-14-2 C6H12O2
RTECS # TZ3500000 Masi ya molekuli: 116.2
UN # 1993
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 33°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 33°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-30GF1-III
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi. Baridi. Kavu. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ISOPROPYL GLYCIDYL ETHER ICSC: 0171
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na hewa au mwanga dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, amini na asidi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA, 75 ppm kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 3B, (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo zaidi ya OEL husababisha kupungua fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 137°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.92
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 19
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 1.25
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.15
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.04
Kiwango cha kumweka: 33°C c.c.
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: tazama Vidokezo
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.5
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005