IODINE ICSC: 0167
Aprili 2004

Jod
Iode
Iodio
Yodo
CAS # 7553-56-2 I2
RTECS # NN1575000 Masi ya molekuli: 253.8
UN #
EC # 053-001-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usigusishe na dutu ziwakazo.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
Macho Kutoa machozi. Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mvuke iso-kikaboni, na za halojeni.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 20/21-50
S: (2-)-23-25-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
IODINE ICSC: 0167
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE KIBLUU NYEUSI AU ZAMBARAU ILIYOKOZA YENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Iodini hujisablimisha mara moja.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na poda ya metali, stibi, amonia, asetaldehide, asetilini kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm; (kiwango cha juu); (ACGIH 2004).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2005).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji, na inakera ngozi. Kuvuta pumzi kwenye mvuke kunaweza kusababisha kuathiri njia za hewa sizifanye kazi vizuri, ugonjwa kama athma (RADS). Kuvuta pumzi kwenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mara chache mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha kushindwa kupumua (RADS). Dutu hii huweza kuathiri thioridi/kikoromeo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 184°C
Kiwango myeyuko: 114°C
Uzito wiani (maji = 1): 4.9
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.03
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0.04
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 8.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.49
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki.
VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005