| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kikohozi. Kuumwa koo. Kichefuchefu. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Huduma ya kusaidia kupua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Uingizaji hewa. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Ainisho ya EU Alama: F+, T+, N R: 12-26-50 S: (1/2-)-9-16-36-38-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-20G2TF au 20S1053 Msimbo wa NFPA : H 4; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Install continous monitoring system with alarm.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI YA MAYAI YALIOOZA. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi sumu (oksidi za sulfuri). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali yote na baadhi ya plastiki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 10 ppm kama TWA; 15 ppm kama STEL; (ACGIH 2004). MAK: 10 ppm, 14 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo huweza kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -60°C Kiwango myeyuko: -85°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.5 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.19 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 260°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 4.3-46 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Dutu hii husababisha upungufu wa kutofautisha harufu. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||