| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Dutu hii huweza kuiwasha moto vitu vile vinavyochomeka. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usigusishe na .vinavyoweza kuwaka au vinakisishaji. Usigusishe na nyuso za moto.
|
Moto unapotokea katika eneo: maji mengi, mnyunyizio wa maji.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapokanzwa au inapogusana na vichoceo vya metali.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Inababua. Madoa meupa kwa ngozi. Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Inababua. Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuumwa koo. Maumivu ya tumbo. Kufura kwa tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Osha kioevu kilichomwagika kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Maunzi maalum. Ainisho ya EU Alama: O, C R: 5-8-20/22-35 S: (1/2-)-17-26-28-36/37/39-45 Angalia: [B] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1 Jasara tanzu za UN: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-51S2015 Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 3; OX |
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho, besi kali, metali. Baridi. Weka gizani. Hifadhi katika viwekeo vinavyopitisha hewa. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapopata joto au inapoathiriwa na mwanga huzalisha oksijeni, ambayo huongeza athari ya moto. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, kusababisha athari ya moto na mlipuko, hasa pakiwepo na metali. Hushambulia dutu nyingi za kikaboni, mfano nguo na karatasi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm kama TWA; A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); (ACGIH 2004). MAK: 0.5 ppm, 7.1 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Aina ya sarakani: 4; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2005). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho na ngozi. Mvuke huu inakera njia ya upumuaji. Dutu hii ikimezwa huweza kusababisha kiputo cha oksijeni kwa damu na mshituko. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mapafu huweza kuathiriwa kwa kuvuta hewa iliyokolea mno. Dutu hii huweza kuathiri nywele, kusababisha kupausha. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 141°C (90%), 125°C (70%)°C Kiwango myeyuko: -11°C (90%), -39°C (70%)°C Uzito wiani (maji = 1): 1.4 (90%), 1.3 (70%) Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.2 (90%), 0.1 (70%) Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.36 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. RTECS MX900000 hidrojeni peroksaidi, mmumunyo wa majimaji >90%; MX0887000 hidrojeni peroksaidi, mmumunyo wa majimaji >30%. Namba zingine za muungano wa mataifa (UN) 2014 (hidrojeni peroksaidi, mmumunyo wa majimaji 20-60%): ainisho ya hatari 5.1, jasara tanzu za UN 8, kikundi ufungashaji cha UN II; 2984 (hidrojeni peroksaidi, mmumunyo wa majimaji 8-20%): ainisho ya hatari 5.1, kikundi ufungashaji cha UN III.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||