| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Inababua. Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. Inababua. Mibabuko ya ngozi nzito. Maumivu.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Inababua. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: T, C R: 23-35 S: (1/2-)-9-26-36/37/39-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-20S1050 Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 1; |
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vioksidishaji vikali, besi kali, metali. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Baridi. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI, YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo katika maji ni asidi kali humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kutoa gesi yenye sumu (klorini - tazama ICSC 0126). Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 ppm (Kiwango cha juu) A4; (ACGIH 2004). MAK: 2 ppm, 3.0 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ukolezi mkubwa wa gesi kunaweza kusababisha kichomi na kuvimba kwa mapafu kuathiri njia za hewa kusababisha sizifanye kazi vizuri (RADS) (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mapafu kusababisha ukamba wa muda mrefu. Dutu hii huweza mmunyo wa meno. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -85°C Kiwango myeyuko: -114°C Uzito wiani: 1.00045 g/l (gesi) Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 30°C: 67 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.3 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.25 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Nambari nyingine za UN: 2186 (kioevu baridi mno) ainisho ya hatari: 2.3; jasara tanzu za UN: 8; 1789 (asidi hidrokloriki) ainisho ya hatari: 8, kifundi ufungashaji cha UN II au III. Mchanganyiko wa majimaji huweza kuwa na hidrojeni ya kloridi kiasi cha thelathini na nane kwa mia (38% ).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||