HEXAMETHYLPHOSPHORIC TRIAMIDE ICSC: 0162
Oktoba 1994

Hexamethylphosphoramide
Hexamethylphosphamide
HMPA
CAS # 680-31-9 C6H18N3OP / {(CH3)2N}3P(O)
RTECS # TD0875000 Masi ya molekuli: 179.2
UN #
EC # 015-106-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwani ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-46
S: 53-45
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HEXAMETHYLPHOSPHORIC TRIAMIDE ICSC: 0162
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KIMIMINIKA , CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za fosforasi, oksidi za nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (ngozi) A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri mapafu, mafigo na mfumo mkuu wa neva, kusababisha kudidimiza na kuharibika kwa utendaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji, mafigo na uboho. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Huweza kusababisha uharibifu wa kijeni kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 232°C
Kiwango myeyuko: 5-7°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.03
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.18
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 105°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Hexametapol ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005