| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi.
|
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo kooni na kifuani.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo plastiki; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: Xi, N R: 41-51/53 S: (2-)-26-39-61 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Usihifadhi au kusafirisha ndani ya vyombo vilivyopakwa madini ya chuma. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ZISIO NA RANGI HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. Iwapo kavu, huweza kuchajiwa kiumemetuamo kwa kuzinga, upitishaji nyumatiki, umiminaji, nk. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni, oksidi za fosforasi. Hushambulia feri na vyombo vilivyopakwa madini ya chuma. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka kwa kunyunyiza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali macho na inakera kwa upole ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko (hutengana): chini ya 234°C Uzito wiani: 1.7 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 1.2 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.0 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Chumvi za sodiamu, potassiamu na amini huyeyuka haraka katika maji. Roundup (chumvi ya monoisopropili ammonia) na Polado (chumvi ya sesquisodium) ni majina ya kibiashara. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||