| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto. Usigusishe na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali).
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 72°C. Hatari ya moto na mlipuko pamoja na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali).
|
Mfumo funge wa zaidi ya 72°C, uingizaji hewa.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kupumua kwa shida.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vya kioo au chuma laini vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 45-60-21/22-23-36/37/38-68 S: 53-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-II
|
Kinachotenganishwa na besi kali, asidi kali, vyakula na malisho. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, KINATACHO KIDOGO HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapogusana na asidi na besi kali, maji, chumvi (kloridi alumini, kloridi feri) au metali (shaba, zinki), kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 ppm kama TWA A3; (ACGIH 2004). MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa viwango vya juu zaidi ya OEL husababisha kupungua fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko (hutengana): 166°C Kiwango myeyuko: -45°C Uzito wiani (maji = 1): 1.1 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 120 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.15 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0 Kiwango cha kumweka: 72°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 415°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||