ETHYLENE OXIDE ICSC: 0155
Oktoba 2001

1,2-Epoxyethane
Oxirane
Dimethylene oxide
(silinda)
CAS # 75-21-8 C2H4O
RTECS # KX2450000 Masi ya molekuli: 44.1
UN # 1040
EC # 603-023-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko ikiwa ni matokeo ya utenganaji kwa nguvu inapokanzwa.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika. Udhaifu.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Alama: F+, T
R: 45-46-12-23-36/37/38
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1040 au 20GTF
Msimbo wa NFPA: H 2; F 4; R 3;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE OXIDE ICSC: 0155
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kukanza kwa kuathiriwa na asidi, besi, kloridi za metali na oksidi za metali kwa athari ya moto au mlipuko. Dutu hii hutengana kama hewa haiko inapokanzwa zaidi ya 560°C, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo mingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; A2; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi endapo ni mmumunyo kwenye maji.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mmumunyo wa maji inaweza kusababisha uwati wa ngozi. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. Yaweza kusababisha dhuru aina ya jenetiki kwa mbegu ya uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 11°C
Kiwango myeyuko: -111°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 146
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.5
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 429°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3-100
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005