ARGON ICSC: 0154
Mei 2003

(kilichooevuka, kilichopozwa)
CAS # 7440-37-1 Ar
RTECS # CF2300000 Masi ya atomi: 39.95
UN # 1951
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Msongo wa hewa.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1951
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ARGON ICSC: 0154
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI KILICHOEVUKA, ISO HARUFU, ISO RANGI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: Kinacho nyima pumzi sahili, (ACGIH 2003).
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Isipodhibitiwa gesi hii huweza kusababisha kukosekana hewa kwa kupunguza kiasi cha oksijeni hewani katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -185.9°C
Kiwango myeyuko: -189.2°C
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 3.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.66
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.94
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Nambari nyingine ya UN: 1006 Argon, iliyobanwa. Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005