| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda kavu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F+, Xi R: 12-36/37 S: (2-)-16-26-29 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2F Msimbo wa NFPA: H 3; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na vikaboni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi zisizo na feri, na plastiki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 ppm kama TWA; 15 ppm kama STEL; (ngozi); (ACGIH 2002). MAK: 5 ppm; 9.4 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2) Ainisho ya MAK: Aina ya mimba: IIc (2002) EU OEL: 5 ppm; 9.4 mg/m³; (EU 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 16.6°C Kiwango myeyuko: -81°C Uzito wiani (maji = 1): 0.7 (kioevu) Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 121 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.55 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.66 Kiwango cha kumweka: -17°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 385°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.5-14 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.27/-0.08 (imekadiriwa) | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ethiliamini husambazwa pia ikiwa 50-70% mmumunyo wa maji (UN 2270). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||