ETHANOLAMINE ICSC: 0152
Oktoba 2002

2-Hydroxyethylamine
2-Aminoethanol
CAS # 141-43-5 C2H7NO / H2NCH2CH2OH
RTECS # KJ5775000 Masi ya molekuli: 61.1
UN # 2491
EC # 603-030-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 85°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 85°C, uingizaji hewa.

MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Katisha kioevu kilichomwagika kwa uangalifu. Kisha osha kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 20/21/22-34
S: (1/2-)-26-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC7-II+III
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, alumini, vyakula na malisho. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHANOLAMINE ICSC: 0152
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI, KISICHO RANGI, KINATACHO, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi pamoja na oksidi za nitrojeni. Dutu hii ni besi kali ya kati. Humenyuka pamoja na nitrati selulosi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali na vioksidishaji vikali. Hushambulia shaba, alumini na aloi zake, na mpira.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: kama TWA 3 ppm; kama STEL 6 ppm (ACGIH 2004).
MAK: 2 ppm 5.1 mg/m³ Sh; Aina ya kiwango cha juu: I (2); Ainisho ya MAK: Aina ya mimba C (2004)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kwa kumeza na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa njia ya upumuaji, ngozi na macho. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 171°C
Kiwango myeyuko: 10°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.02
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 53
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 85°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 410°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.5-17
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.31 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005